Hamia kwako na Watumishi Housing Company, Tanzania

Trump aelezea sera zake za kigeni kwa gazeti la Marekani

Trump amesema Uingereza wamefanya vizuri kujitoa ndani ya umoja wa ulaya
Image captionTrump amesema Uingereza wamefanya vizuri kujitoa ndani ya umoja wa ulaya
Rais mteule wa Marekani Donald Trump, ametoa ufafanuzi juu ya vipaumbele vyake katika sera zake za kigeni katika mahojiano na gazeti la Times la Uingereza na gazeti la Bild la Ujerumani.
Trump amesema anataka mipango ya biashara yenye usawa kwa Marekani kutoa mipango yake ya biashara na nchi nyingine duniani hususani China.
Katika uongozi wake anatilia mkazo suala la biashara yenye tija zaidi kuliko biashara huru.
Alirudia na kusisitiza kwamba kampuni kubwa za kibiashara nchini Marekani zilizowekeza nje ya Marekani zitakabiliana na ushuru mkubwa wa bidhaa wanazotaka kuuza nchini Marekani.
Katika mahojiano hayo yaliyofanyika katika ofisi yake iliyopo kwenye jengo la Trump, amesema Kansela wa Ujerumani ni kiongozi bora Ulaya
Image captionKatika mahojiano hayo yaliyofanyika katika ofisi yake iliyopo kwenye jengo la Trump, amesema Kansela wa Ujerumani ni kiongozi bora Ulaya
Trump amesema kwamba angependa Urusi na Marekani wakubaliane kupunguza kwa kiasi kikubwa silaha za kinyuklia kwa kubadilishana na kusitisha vikwazo huko Moscow.
Kwa upande wa Mashariki ya kati amesema mahusiano mazuri yangetakiwa kuundwa nchini Syria na kusimamiwa na washirika wa Marekani.
Trump pia amesema kansela wa Ujerumani Angela Merkel amefanya kosa kubwa alipowaruhusu wakimbizi wengi kutoka Syria na mataifa mengine kuingia nchini Ujerumani.
SOURCE BBC SWAHILI
Share on Google Plus

About Ngoma Kali Tz

0 comments:

Post a Comment