Hamia kwako na Watumishi Housing Company, Tanzania

Trump alaumiwa kuhusiana na matokeo ya uchaguzi wa Marekani

Zoezi la Upigaji kura Marekani

Watu maarufu kutoka chama cha Republican nchini Marekani wamemlaumu Rais Donald Trump kwa kurudia madai yake kwamba alishindwa kura za jumla na mshindani wake Hillary Clinton kwa sababu karibu watu milioni 3 walipiga kura kinyume cha sheria.
Awali, Seneta wa Republican Lindsey Graham amesema maneno hayo ya Rais Trump kutuhumu wapiga kura pamoja na aliyekuwa mpinzani wake wakati wa uchaguzi, hayafai kuzungumzwa na Rais bila ya uthibitisho.
Naye Spika wa Bunge Paul Ryan, amesema pia Rais Trump anapaswa kuacha kutoa malalamiko ambayo hayajathibitishwa.
Kwa upande wao chama cha Democrats pia kimeyakosoa madai hayo.
Kiongozi wa chama hicho katika Bunge la Senate Chuck Schumer amesema Donald Trump anahitaji kuangazia zaidi utawala wake mpya.
Amesema badala ya kuzungumzia uchaguzi au ni watu wangapi walijitokeza katika siku ya kuapishwa anapaswa kuzungumzia ni ajira ngapi atakazozitengeneza.
Amesisitiza kuwa ni wakati yeye wa kuwa Rais sasa. Wakati uongo huu ulipozungumzwa, wenzetu wa Republican walikuwa na wajibu wa kukataa..''
Hata hivyo msemaji wake amesisitiza kwamba Rais Trump ataendelea kuamini tuhuma hizo.
Rais Trump, ambaye aliyatoa malalamiko hayo kwa mara ya kwanza mwishoni mwa mwezi Novemba kupitia Twita, mpaka sasa bado hajatoa ushahidi wowote juu ya madai yake hayo.
Share on Google Plus

About Ngoma Kali Tz

0 comments:

Post a Comment