Hamia kwako na Watumishi Housing Company, Tanzania

Yanga yashughulikiwa na Azam bila huruma


Na Zainab Nyamka,
 Globu ya Jamii, Zanzibar
Timu ya Azam Fc imefanikiwa kuingia hatua ya nusu fainali kwa kuipa kipigo cha mbwa mwizi cha bao 4-0  timu ya Yanga huku wakikalia usukani mwa kundi B katika kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar usiku huu.

Mpira ulianza kwa kasi ikionekana Azam FC wamepania kupata bao la mapema Dakika ya kwanza ya mchezo na katika dakika ya 2 Azam wanapata bao kupitia kwa mfungaji wao John Bocco baada ya  kutokuwa na maelewano baina ya mabeki wa Yanga kwenye kuuokoa mpira uliookolewa na golikipa wa Yanga, Deogratius Munish "Dida".

Katika dakika ya 9 Yanga wanafanya shambulizi langoni mwa Azam lakini Saimon Msuva anashindwa kumalizia kazi nzuri iliyofanywa na mrundi Amisi Tambwe.

Baada ya kuonekana kutokuwa na maelewano katika safu ya ushambuliaji Kocha George Lwandamina anafanya mabadiliko kwa kumtoa  Juma Mahadhi na nafasi yake inachukuliwa na Emmanuel Martin katika dakika ya 36. Mpaka Mapumziko Azam 1 Yanga 0.
Kipindi cha pili kinaanza kwa kila mmoja kumsoma mwenzake lakini katika dakika ya 54, Yahaya Mohamed  anaipatia Azam goli la pili baada ya kuunganisha krosi safi Abubakar Salum " Sure Boy".


Wakiwa bado hawaamini Dk 81, Joseph Mahundi anaiandikia Azam goli la tatu baada ya kuachia shuti kali nje ya 18 na kuacha mashabiki wa Yanga wakiduwaa wakiwa hawaamini wanachokiona.
Dk 84, Atta aliyeingia kipindi cha pili anaifungia timu yake bao safi akiunganisha  pasi ya Afful baada ya Mwashiuya kuukosa mpira, na mpaka mpira unamalizika Azam wanatoka kifua mbele wakiwa na alama 7 wakifuatiwa na Yanga wenye alama 6.  
Timu hizi zinasubiri washindi wa mechi za kesho kwenye kundi A ili kupambana nazo kwenye hatua ya nusu fainali.

Kikosi cha Yanga kilichopambana usiku huu.


Kikosi cha Azam kilichopambana usiku huu.
 Timu zikiingia uwanjani wakati wa mchezo wa hatua ya makundi kati ya Yanga na Azam 
 Saimon Msuva akimtoka beki wa Azam wakati wa mchezo wa hatua ya makundi wa kombe la Mpoinduzi uliomalizika kwa Azam kutoka na ushindi wa goli 4-0.
 Juma Mahadhi akipambana katikati ya mabeki wa Azam wakati wa mchezo wa hatua ya makundi wa kombe la Mpoinduzi uliomalizika kwa Azam kutoka na ushindi wa goli 4-0.

SOURCE -MICHUZI BLOG
Share on Google Plus

About Ngoma Kali Tz

0 comments:

Post a Comment