Hamia kwako na Watumishi Housing Company, Tanzania

Jamaa auza mgongo wake

Auza mgongo wake kwa mchoraji
Tim Steiner ana mchoro mkubwa aina ya tattoo mgongoni mwake. 

Alichorwa na msanii mmoja mashuhuri mbelgiji aitwae Wim Delvoye
Na mchoro huo japo uko mgongoni mwake uliuzwa na ukanunuliwa na mkusanyaji sanaa kutoka Ujerumani, Rik Reinking.

Tena, kuna makubaliano- kwamba Steiner atakuwa akikaa mgongo wazi kwenye maonyesho akinadi mchoro huo, na hatimae Steiner atakapofariki basi ngozi yake itatundikwa kwenye fremu kwa ajili ya maonyesho zaidi.

"ndio; Kazi hiyo ya usanii iko mgogoni mwangu, mie nainadi tu " Steiner mwenye umri wa miaka 40 amenukuliwa akisema.
Nguruwe waliochorwa tatoo
Steiner mwenyewe aliwahi kufanya kazi kama meneja wa duka la uchoraji tattoo huko Zurich lakini mpango huo wote ulifanikishwa na rafikie wa kike ambae ndiye aliyemfahamisha kwa mchoraji huyo wa ubelgiji Wim Delvoye, aliyekuwa akitafuta mtu ili atekeleze wazo lake hilo tata la kumchora mtu tatoo mgongo mzima kwa ajili ya kuiuza.

Delvoye alikuwa akifahamika vyema kwa mtindo wake mwengine tata wa kuchora tatoo kwenye migongo ya nguruwe.
Steiner anasema siku mpenziwe alipomwelezea jambo hilo hakusita kamwe -akajibu kwamba yuko tayari.
''mimi sasa ngozi niliyonayo si yangu, inamilikiwa na Rik Reinking - mgongo wangu ni kama 'canvas' tu ya kuchorea ''anaeleza Steiner kama vile mzaha!
Mchoro wa tattoo
Mchoro huo ulichukua saa 40 kumalizika- na unajumisha vitu vya kawaida kama maua aina ya waridi na mengineyo , samaki wanaopatikana sana huko Uchina waitwao koi, picha za watoto, mchoro wa mwanamke anaefanana na Madona lakini pia mchoro ulio na utata zaidi wa fuvu la kichwa cha mwanadamu.

Saini ya msanii iko upande wa kulia wa mchoro huo.
'Kweli ni mchoro mzuri na wa ajabu , mie naupenda ," Steiner anasisitiza .

Mchoro huo unaoitwa TIM, uliuziwa mjerumani Rik Reinking hapo 2008 kwa pauni £130,000 za Uingereza na Steiner akalipwa theluthi moja ya fedha hizo.

"Watu wengi wanaponiona nimekaa kwenye maonyesho nikiwa nimetulia wanadhani ni sanamu, kisha wanashangaa sana wakiniona ni binadamu aliye hai.'' Steiner anaendelea kueleza.
Steiner akikaa mgongo wazi ili kuunadi mchoro huo
Hata hivyo mchoro huo huzua mijadala mikali , baadhi ya wanaoiona wakisifia lakini wengine wanafananisha jambo hilo na ukiukaji wa haki za kibinadamu na hata kuuita utumwa.
Lakini hilo halimbabaishi kamwe Steiner kwani mkataba wake unasema anapaswa kukaa kwenye maonyesho angalau mara 3 kwa mwaka.
Mara ya kwanza alishiriki maonyesho ya Zurich mwezi Juni 2006 .
Lakini mwaka jana wakati wa sherehe ya kuadhimisha miaka 10 tangu tatoo hiyo kuchorwa ilimbidi kuwa katika makavazi kwa kipindi kirefu zaidi -saa 5 kwa siku kwa situ 6 kila wiki ,kwa mwaka mzima kwenye makavazi yaitwayo Museum of Old and New Art (Mona) huko Hobart, Tasmania.
Steiner akiunadi mchoro huo 2012
Ratiba hiyo ndefu iliisha mwanzoni mwa wiki .
''Ilinibidi nikae kwenye maonyesho zaidi ya saa 1500 ! Ilikuwa kazi kweli, wakati mwengine ni kama mwili hauwezi kabisa unataka kujiangusha ulale lakini nilivumilia na kukaa chonjo kila wakati, hiyo ndio kazi yangu..hayo ndiyo maisha yangu ! "anasema Steiner.

Japo kuna uzio uliowekwa watu wasimfikie , wengine wamewahi kuuvuka na kwenda kumgusa , huku wengine wakipiga mayowe na baadhi hata kumtemea mate.
Hata hivyo hata watu wakimsemea na kumuuliza maswali , yeye huwa hajibu chochote, anakaa tu kimya na kutulia.

Kuna wakati hata ilibidi Steiner kufanyiwa operation mbili za mgongo kutokana na maradhi ya mifupa ya mgongo yaliyomkumba kutokana na hali hiyo ya kukaa kwa vipindi virefu kwenye maonyesho ya sanaa.
Share on Google Plus

About Ngoma Kali Tz

0 comments:

Post a Comment