Hamia kwako na Watumishi Housing Company, Tanzania

Kiongozi wa upinzani nchini Rwanda atangaza kuunda serikali yake


media 
 
Hali ya sintofahamu imeripotiwa nchini Rwanda baada ya kasisi wa zamani ambaye kwa sasa ni kiongozi wa upinzani nchini humo Thomas Nahimana, kutangaza kuunda serikali sambamba na utawala uliopo Rwanda.
Hata hivyo kiongozi huyo amesema kuwa serikali yake itakua ikifanyia uhamishoni.

Uamuzi huo umechukuliwa baada ya Thomas Nahimana, kupigwa marufuku kuingia Rwanda kujiandikisha kama mgombea wa kiti cha urais katika uchaguzi mkuu unaopangiwa kufanyika mwezi Agosti mwaka huu.

Kiongozi huyo wa upinzani aliye uhamishoni anasema lengo la serikali yake ni kuiondoa madarakani serikali ya Rais Paul Kagame. Thomas Nahimana ameushtumu utawala wa Paul Kagame kwamba unavunja sheria na kukandamiza wananchi.

Thomas Nahimana kwa sasa anayeshi nchini Ufaransa na amesema kuwa serikali yake itakayofanyia kazi nje ya nchi.

Hivi karibu Thomas Nahimana alitarajiwa kurejea nchini Rwanda akitokea jijini Brussels nchini Ubelgiji, lakini hakuweza kufanya hivyo baada ya kudai kuwa serikali ya Kigali inaendelea kumwekea vikwazo.

Mwanasiasa huyo ambaye anatumia pasi ya usafiri ya Ufaransa, tayari ametangaza nia ya kuwania urais nchini humo mwezi Agosti mwaka huu.

Mwezi Novemba mwaka uliopita, alizuiliwa jijini Nairobi nchini Kenya wakati anajiandaa kuabiri ndege kwenda jijini Kigali, baada ya serikali ya Rwanda kuitaka Kenya kutomruhusu kufika Kigali.

Yves Butera, msemaji wa Idara ya Uhamiaji nchini Rwanda wakati huo alisema kuwa Padri huyo atakaribishwa nchini Rwanda kama raia mwingine.
Share on Google Plus

About Ngoma Kali Tz

0 comments:

Post a Comment