Hamia kwako na Watumishi Housing Company, Tanzania

Samatta aweka rekodi mpya ulaya

Baada ya ushindi wa goli 5-2 wa KRC Genk ugenini katika mchezo wa kwanza wa Europa League hatua ya 16 bora dhidi ya KAA Gent, leo March 16 2017 walirudiana na tena na KAA Gent katika uwanja wa Luminus Arena, Genk walikuwa wenyeji lakini walikuwa wanahitaji walau sare tu kufuzu robo fainali. KRC Genk sasa wamefuzu kucheza robo fainali ya UEFA Europa League baada ya game ya leo kumalizika kwa sare ya 1-1, hivyo Genk wanaiondoa KAA Gent kwa jumla ya goli 6-3, mtanzania Mbwana Samatta anaingia kwenye rekodi ya kuwa mtanzania kufikia hatua hiyo ya robo fainali. Hadi sasa timu zilizofuzu kucheza robo fainali ya UEFA Europa League ni KRC Genk, Besiktas na Celta Vigo na timu tano nyingine zilizofuzu zitajulikana baada ya michezo ya usiku wa leo ambapo baadhi yao inachezwa usiku huu, baada ya kujulikana timu nane usiku huu, kesho ndio itachezeshwa droo ya robo fainali.
Share on Google Plus

About Ngoma Kali Tz

0 comments:

Post a Comment