Hamia kwako na Watumishi Housing Company, Tanzania

Malkia Elizabeth II kuadhimisha miaka 91

mediaElizabeth II, Malkia wa Uingereza, hapa katika mji wa Plymouth, mwezi Machi mwaka 2015.REUTERS/Matt Cardy/Pool
Malkia Elizabeth II, ambaye anaadhimisha miaka 91 Ijumaa hii Aprili 21, ameagiza wajumbe wengine kutoka familia yake ya kifalme kumuwakilisha katika mamlaka yake mengine. Lakini afya ya kiongozi huyo kongwe nchini Uingereza inaendelea kuzorota.
Kama kila mwaka, siku ya kuzaliwa ya Malkia, itasheherekewa huku mizinga 41 ikipigwa katika Hyde Park na mingie 62 katika mnara wa London.
Malkia Elizabeth II ambaye alizaliwa Aprili 21, 1926, huwa akisherehekea siku yake ya kuzaliwa katika hatua mbili: katika tarehe ambayo alizaliwa, na katika sherehe rasmi ya mwezi Juni, kulingana na mila za kale na lengo la kuepuka machafuko ya hali ya hewa .
"Bado niko hai," alisema Malkia miezi miwili iliyopita wakati wa ziara yake nchini Ireland ya Kaskazini.
Itafahamika kwamba Malkia Elizabeth II ametimiza miaka 65 akiwa kiti cha enzi nchini Uingereza.
Share on Google Plus

About Ngoma Kali Tz

0 comments:

Post a Comment