Hamia kwako na Watumishi Housing Company, Tanzania

UBADHIRIFU WA FEDHA UNAUA VYAMA VYA USHIRIKA CHUNYA-Rc Makalla

 Displaying Screenshot_2017-05-09-13-19-46-1.png
 Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mh, AMOS GABRIELY MAKALLA wa tatu kutoka kulia akiwa na mkuu wa wilaya ya chunya REHEMA MADUSA.

Mkuu wa mkoa wa mbeya Mh, AMOS GABRIELY MAKALLA Amesema uendeshaji vyama vya ushirika bila kuzingatia sheria ni hatari na ndiyo chanzo cha ubadhirifu na kuua ushirika

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa mafunzo Kwa viongozi wa Chama cha ushirika wa zao la Tumbaku wa Wilaya ya Chunya na Songwe na kuwataka wajenge ushirika wenye nguvu, waepuke ubaridhirifu na kufuata sheria za ushirika katika uendeshaji wa shughuli zao za kila Siku.

Aidha amevitaka vyama vya ushirika vijiendeshe kwa kufuata sheria, vijenge imani kwa wanaushirika na kuweka wazi taarifa za fedha

MAKALLA ameongeza kwa kusema kuwa warajisi wa ushirika kuwa wepesi kushughulikia matatizo ktk vyama vya ushirika na amemwomba Mrajisi Mkuu wa ushirika kufanya mafunzo kama hayo kwa VIONGOZI wa vyama vyote vya ushirika na maafisa ushirika wa halmashauri zote za Mkoa wa Mbeya.
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment