Hamia kwako na Watumishi Housing Company, Tanzania

MKOA WA MBEYA KUWA LANGO LA UCHUMI NA UTALII NYANDA ZA JUU KUSINI. 
  Mkuu wa mkoa wa mbeya Mh AMOS GABRIELY MAKALLA katikati akiwa  kwenye kikao na viongozi wengine wa mkoa(hawapo pichani).

Mkuu wa mkoa wa mbeya Mh AMOS GABRIELY MAKALLA amesema katika jitihada za kutatua changamoto za wananchi kupitia vikao vya ndani mkoa umeonyesha mabadiliko makubwa kwa kushirikiana na wananchi.

Mh MAKALLA  ametoa kauli hiyo alipokuwa kwenye kikao chake na viongozi wa ndani katika kutoa tathimini ya mwaka mmoja ya uongozi ambapo ameitaja mikakati ya kuifanya mbeya kuwa lango la uchumi na utalii katika mikoa ya nyanda za juu kusini.

Mikakati iliyotajwa na mkuu huyo wa mkoa wa mbeya kupitia kikao hicho kuwa ni pamoja na kukamilika kwa meli mbili za mizigo na  moja ya abiria katika bandari ya kiwira, kutumika kwa uwanja wa ndege za kimataifa wa songwe, kuwepo kwa barabara inayounganisha nchi za Malawi na ukanda wa nchi za afrika kusini pamoja na vivutio vya utalii Hifadhi ya ruaha, kitulo na katavi.

Pamoja na vivutio hivyo mkuu wa mkoa wa mbeya ameongeza kuwa serikali itaendelea kuzitafutia ufumbuzi kero za wananchi ikiwa ni pamoja na kuhamasisha wananchi masuala ya kilimo na mafuzo ya  ujasiriamali ili kutekeleza kwa vitendo sera ya viwanda, uwezeshaji wananchi kiuchumi, elimu na afya.
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment