Hamia kwako na Watumishi Housing Company, Tanzania

RC MAKALLA AWAPONGEZA WAANDISHI WA HABARI MBEYA KUJILIPIA BIMA YA AFYA
 Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Mkalla akizungumza na waandishi wa Habari mkoa wa Mbeyaasubuhi hii ya leo.
 Kulia ni makamu Mwenyekiti wa Chama cha waandishi wa habari mkoa wa Mbeya Hoseah Cheyo, akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Gabriel Makalla kifimbo ambacho baadhi ya waandishi wa habari waliotembelea hivi karibuni Kijijini Butiama mkoani Mara katika makumbusho ya Mwalimu Nyerere walikitoa huko.
 Kulia ni makamu Mwenyekiti wa Chama cha waandishi wa habari mkoa wa Mbeya Hoseah Cheyo, akizungumza kwa niaba ya waandishi wa habari wa mkoa huo.


Mwakilishi wa Meneja wa mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa, Haji Mpete.Mwakilishi wa Mganga mkuu wa Mkoa wa Mbeya Dr. Agness Buchwa, akizungumza na waandishi wa habari katika hafla fupi ya kuwakabidhi kadi za bima ya afya ya Taifa baadhi ya waandishi wa habari wa mkoa wa Mbeya.


Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla akimkabidhi kadi ya bima ya Afya ya mwandishi wa habari Aines Thobias katika ukumbi wa Coffee Garden Jijini Mbeya leo.

NA SAM MHANDO 

MKUU wa Mkoa wa Mbeya Amos Gabriel Makalla, amewapongeza waandishi wa habari mkoa wa Mbeya kwa uamuzi wao wa kuhamasishana kuchangia na kupatiwa kadi za bima ya Afya ya Taifa (NHIF).

Pongezi hizo zimetolewa leo katika ukumbi wa Coffee Garden mjini Mbeya alipokuwa akikabidhi kadi za bima ya Afya kwa baadhi ya waandishi wa habari Jijini Mbeya.

Makalla amesema waandishi wa habari wanafanya kazi kubwa katika Taifa na waandishi wa mkoa wa Mbeya wameamua kujitambua zaidi na kutambua kuwa matatizo hayaji kwa kupenda ikiwemo Kifo, Kuugua na uzee.

“Niwakumbushe wamiliki wa vyombo vya habari kuwawekea mazingira mazuri waandishi wao na kwamba kuna msemo unaosema kuwa ukondefu wa mbwa ni aibu kwa mwenye mbwa hivyo kutapatapa kwa waandishi wa habari ni aibu kwa wamiliki” alisema Makalla.

Aliomba waandishi kuendeleza uzalendo wao ikiwa ni pamoja na kuhamasisha wananchi kujiunga na bima za afya ikiwemo mfuko wa bima ya afya ya jamii (CHF).

Kwa upande wake makamu mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Mbeya Hoseah Cheyo alimwambia Mkuu wa mkoa kuwa pamoja na mambo mengine, waandishi wa habari wanampongeza Rais Dkt. John Magufuli kwa kazi kubwa anazoendelea kuzifanya kwa ajili ya Taifa.

Katibu Mkuu wa chama hicho alisema kuwa waandishi wa habari wamehamasishana wenyewe katika kupata michango na kulipia kadi hizo.
 
alisema kwa sasa Hospitali za mkoa wa Mbeya hususani Hospitali ya Mkoa na Rufaa, wametenga maeneo maalum kwa ajili ya watu wanaotibiwa kwa njia za kadi za bima ya Afya.

Mwakilishi wa Meneja wa mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa, Haji Mpeta alisema kuwa matibabu ni ghali hivyo waandishi waliolipia kadi za bima ya Afya wataweza kupata matibabu katika vituo 6500 kote nchini kwa gharama ya Tsh. 76,800 kwa mwaka.
 
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment