Hamia kwako na Watumishi Housing Company, Tanzania

CCM, MKOA WA NJOMBE WAPATA MWENYEKITI MPYA JAH, PEOPLE AFUNGUKA,


Mwenyekiti mpya wa CCM Mkoa wa njombe Mh, Jassel Mwamwala mwenye mataji Shingoni akishangilia ushindi Akiwa na Mbunge wa jimbo la Lupembe Mh, Joramu Hongoli Kulia.
Mwenyekiti wa ccm Mkoa wa Jombe aliyemaliza muda wake Mh, Deo Sanga, Jah People Akizungumza na wapigakura
Baadhi ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM mkoa wa Njombe wakiwa Ukumbini Kwaajili ya Uchaguzi
Mwenyekiti Mpya Mh, Jassel Mwamwala Akiwa Amebebwa na wapigakura Baada ya Kutangazwa kuwa mshindi wa Nafasi ya Mwenyekiti wa Mkoa wa Njombe
Mwenyekiti mpya wa CCM mkoa wa njombe akiwa amekumbatiana na Mwenyekiti aliyemaliza muda wake
Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa NEC ,Mkoa wa Njombe Bw, Fidelis Lumato akiwashukuru wajumbe kwakumpa nafasi hiyo,

Na Maiko Luoga NJOMBE,

Wajumbe wa Mkutano mkuu wa chama cha mapinduzi mkoa wa Njombe hapo jana November 5 mwaka huu walichagua viongozi wa chama hicho akiwemo mwenyekiti wa CCM Mkoa ,Mjumbe wa halmashauri Kuu ya Taifa NEC pamoja na Katibu wa siasa na Uenezi wa Mkoa wa Njombe.

Mkutano huo mkuu wa Mkoa ulimchagua Mh, Jassel Job Mwamwala kuwa Mwenyekiti wa Mkoa wa Njombe, na Bw,Fidelis Lumato Kuwa Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa NEC Pamoja na Bw,Erasto Ngole Kuwa Katibu wa siasa na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi CCM mkoa wa Njombe. 

Awali chama cha mapinduzi CCM Mkoa wa Njombe kilikuwa kikiongozwa na Mwenyekiti aliyemaliza muda wake na Mbunge wa Makambako Mh, Deo Sanga Jah People ambae kwa sasa Katiba ya chama hicho inamruhusu mh, Deo Sanga kubaki na nafasi moja ya Ubunge katika jimbo la Makambako licha ya Kugombea nafasi hiyo na Kamati kuu ya CCM tTaifa NEC Haikurejesha Jina lake.

Akizungumza kwa niaba ya Viongozi waliochaguliwa hapo jana katika mkutano mkuu wa CCM Mkoa wa njombe uliofanyika katika ukumbi wa shule ya Sekondari Hagafilo Mwenyekiti mpya wa CCM Mkoa wa Njombe Mh,Jassel Job Mwamwala aliwashukuru wajumbe waliofika kuwachagua viongozi hao kutoka katika wilaya za Ludewa, Njombe, Wanging’ombe Pamoja na Makete.

Aidha mkutano huo pia uliwachagua wajumbe wawili kutoka kwenye kila wilaya za Mkoa wa Njombe watakaounda Halmashauri kuu ya Mkoa ambapo wajumbe waliochaguliwa kutoka wilaya ya Ludewa ni Bw,Vasco Mgimba pamoja na Mzee Thobias Thobias Ligala ambae pia alichaguliwa na Halmashauri kuu ya Mkoa kuwa Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Njombe.
 
Mkutano huo mkuu wa uchaguzi wa Chama cha mapinduzi CCM Mkoa wa njombe uliendeshwa na kusimamiwa na Msimamizi mkuu wa uchaguzi huo Mh,Pereilla Silima ambae ni Katibu wa Halmashauri kuu ya Taifa Organization.
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment