Hamia kwako na Watumishi Housing Company, Tanzania

Masoud Kipanya ajitokeza hadharani ‘namshukuru aliyesambaza taarifa’

Mwandishi wa Habari za vikaragosi/Vikatuni nchini Tanzania, Masoud Kipanya amejitokeza hadharani baada ya taarifa za kushikiliwa na watu wasiojulikana kusambaa mitandaoni.
Kipanya amethibitisha taarifa hizo za kupatikana kwake kupitia ukurasa wake wa Twitter ambapo amesema anamshukuru sana mtu aliyesambaza taarifa za kukamatwa kwani ndio zimemuokoa.
Poleni kwa usumbufu na asanteni kwa kujali hali za wengine. Niko salama Alhamdulillah. Namshukuru pia aliyesambaza taarifa. ‘AMESAIDIA’.“ameandika Masoud Kipanya.
Mapema leo Januari 01, 2018, kulizagaa taarifa kwenye mitandao ya kijamii nchini Tanzania kuwa Masoud Kipanya amekamatwa na watu wasiojulikana ambapo hata kampuni ya Clouds Media Groups ilishindwa kutolea maelezo ya kina ya taarifa hizo.
Share on Google Plus

About Ngoma Kali Tz

0 comments:

Post a Comment