Hamia kwako na Watumishi Housing Company, Tanzania

Ukiwa huku ni marufuku kula wala kunywa ukiwa unatembea mtaani, ukikamatwa faini yake ni Tsh milioni 1 (+picha)

Kama wewe ni Mtanzania na umezoea kula au kunywa ukiwa njiani au kwenye misele yako, taarifa hii ikufikie popote pale ulipo duniani, kuwa tabia hiyo sio rafiki tena itakugharimu.
Tourists in pictured, are being warned they could face fines of up to £450 if they eat in certain streets in the city 
Jiji la Florence, Italia
Tabia hiyo sio rafiki tena kwa mji wa Florence nchini Italia ambapo mamlaka husika imetangaza rasmi kuwa watalii na wakazi wa mji huo wa kitalii hawataruhusiwa kula wakiwa wanatembea kwenye mitaa ya mji huo.
Sheria ya kuzuia watu kula njiani au mitaani  imeanza kufanya siku ya jana ambapo muswada wake ulipitishwa miezi minne na ulikuwa unasubiri kusainiwa.
Image result for Florence
Halmashauri ya jiji hilo la kihistoria nchini Italia, imesema kuwa imechukua maamuzi hayo baada ya kuona watalii wengi wanaoingia kutupa taka taka ovyo hasa za Take Away jambo ambalo linapoteza mvuto wa jiji hilo na kuongeza uchafu.
Kwa mujibu wa gazeti la The Local  la nchini Italia, limeeleza kuwa marufuku hiyo itaanza saa 6 mchana hadi saa 4 usiku, na tayari askari wameshapagwa kwenye maeneo ya kazi leo kwenye manispaa nne za jiji hilo ambazo ni; Via de’ Neri, Piazzale degli Uffizi, Piazza del Grano na Via della Ninna.
Related image
Meya wa jiji hilo la kitalii, Dario Nardella, akiongea na gazeti la The Local amesema kuwa lengo la sheria hiyo ni kufanya jiji hilo kuwa safi muda wote kwani kuna watalii ambao huwa wanachafua kwa kutupa taka ovyo ikiwemo chupa za bia na mvinyo.
Image result for dario nardella
Dario Nardella
Hii sio mara ya kwanza kwa Meya huyo kufanya hivyo, kwani mwaka jana aliwataka watu wote watakaoweka mahema ya kusali nje ya makanisa wahakikishe wanasafisha mazingira yao kabla ya kutoka kwenye jiji hilo.
Share on Google Plus

About Ngoma Kali Tz

0 comments:

Post a Comment