Hamia kwako na Watumishi Housing Company, Tanzania

Wizkid atangaza kujenga shule kwa fedha atakazoingiza kwenye dili lake jipya na Nike

Msanii wa muziki kutoka Nigeria, Wizkid ameahidi kujenga shule jijini Lagos nchini humo kwa kutumia fedha atakazoingiza kupitia dili lake jipya na kampuniya mavazi ya Nike.
Wizkid
Wizkid amethibitisha taarifa hizo kupitia ukurasa wake wa Twitter kwa kuandika “Kwa faida ndogo nitakayoipata kupitia ubia wangu wa  kibiashara na Nike nitajenga shule nyumbani Lagos”.

Wizkid aliingia makubaliano ya kibiashara kupitia brand yake ya StarBoy na kampuni ya Nike ambayo inajihusisha na utengenezaji wa vifaa vya michezo mwanzoni mwa mwezi Februari mwaka huu.
Share on Google Plus

About Ngoma Kali Tz

0 comments:

Post a Comment